Latest News and UpdatesPosted On : 2024-02-06


Wanafunzi wenye mahitaji maalum wapewa vifaa


Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu alishiriki kwenye siku maalum iliyoandaliwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum. Siku hii imelenga kuwapa kipaumbele wanafunzi wote wenye mahitaji maalum kwa kuwakumbuka katika kutimiza mahitaji yao mbalimbali.

 Mhe. Zungu aliupongeza uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha kwa namna wanavyowajali wanafunzi hawa wenye mahitaji maalum, na kuangalia namna ya kuwawezesha vifaa mbalimbali ikiwemo Vitimwendo, Mafuta ya Ngozi, Fimbo za kuwaongoza wenye ulemavu wa macho nk. Mhe. Zungu aliahidi kutoa Tsh. Milioni 10 kutoka kwenye fedha za mfuko wa jimbo ili kuchangia zoezi la kununua vifaa mbalimbali vya wanafunzi wenye mahitaji maalum. Alimalizia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyowapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalum kwa kuwapa nafasi kwenye kada mbalimbali.

PAYMENT PORTAL

PROGRAMME BROCHURE

COLLABORATIONS

HEET PROJECT

IFM PROSPECTUS

SHORT COURSES

ALMANAC 2023/2024

CONTACT US

Main Campus
contact our main campus via
P.O Box 3918, 5 Shaaban Robert Street
11101 Dar es salaam
+255 22 2112931-4
Fax : +255 22 2112935
rector@ifm.ac.tz